Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE AZZA ATATUA CHANGAMOTO YA ZAHANATI KIJIJI CHA ISELA..SASA KUANZA KAZI OKTOBA 20,2026




Na Marco Maduhu, Stela Paul, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, ametatua changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Isela, baada ya Zahanati ya kijiji hicho kushindwa kutoa huduma za matibabu licha ya kukamilika kujengwa.

TAZAMA VIDEO👇👇


Ametatua tatizo hilo leo Oktoba 1, 2026, kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji hicho, mara baada ya changamoto hiyo kuwasilishwa katika mkutano huo, ikilalamikiwa kuwa Zahanati hiyo imeshindwa kutoa huduma za matibabu licha ya kukamilika, pamoja na kuletwa kwa watumishi ambao kwa sasa wapo katika Kituo cha Afya Samuye.
Azza amesema ameshafuatilia ili kujua sababu za Zahanati hiyo kutofanya kazi licha ya kukamilika, na kupewa majibu kuwa kunatakiwa kuwapo milango miwili upande wa vyoo, pamoja na kupatikana kwa vifaa tiba.

“Naomba simu yangu nimpigie Mganga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga (DMO), ili atuambie Zahanati hii inafunguliwa lini, sababu hatuwezi kukubali Zahanati imekamilika, na Halmashauri ilikuwa imetenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba,” amesema Azza.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge, akizungumza kwa njia ya simu kwenye mkutano huo, amesema Zahanati hiyo itaanza kutoa huduma kuanzia Oktoba 20 mwaka huu, na watumishi watatu tayari wameshaletwa katika Zahanati hiyo.

Ameongeza kuwa katika bajeti, Halmashauri imeongeza Sh. milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba, na kwamba vifaa tiba vya kuanza navyo vipo.
Naye Diwani wa Samuye, John Ngengeshi, amempongeza Mbunge Azza kwa kutatua changamoto za miradi ambayo ilikuwa viporo, na kumuomba awasaidie kuhakikisha Zahanati ya Kijiji cha Isela inaanza kutoa huduma za matibabu, kwa sababu imekamilika, lakini kumekuwa na chenga nyingi za kuanza kufanya kazi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Isela kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Zahanati ya kijiji hicho.
Diwani wa Samuye John Ngengeshi akizumgumza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com