Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : HOLYSMILE YATIKISA KAHAMA, MDAU SHUPAVU AWARDS SHINYANGA - 2026 ZATOLEWA KWA KISHINDO!


Tuzo za MDAU SHUPAVU Awards – Shinyanga 2026, Season 2, zimetolewa Oktoba 20, 2026, katika ukumbi wa Miligo Hall, mjini Kahama, mkoani Shinyanga.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Taasisi ya HOLYSMILE, chini ya Mkurugenzi wake Arnold A. Bweichum Jr, zinalenga kutambua na kuenzi mchango wa watu binafsi, taasisi na biashara zinazofanya vizuri katika sekta mbalimbali, pamoja na kuhamasisha ubunifu, ujasiriamali, vipaji na utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Tuzo hizo pia zinalenga kuwapa wadau hamasa ya kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga. Washindi walipatikana kupitia kura za wazi katika kategoria mbalimbali zinazohusisha biashara, habari, burudani, elimu, mitindo na urembo, uongozi na maendeleo ya jamii.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com