Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GEITA YALENGA KUWA KITOVU CHA TEKNLOJIA YA MADINI AFRIKA RC MNYETI



Na Sheila Ahmadi, Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexandra Mnyeti amewaalika wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kushiriki Maonesho ya Madini na Teknolojia yanayoendelea mkoani humo, yakilenga kuwaunganisha wadau wa mnyororo wa thamani wa madini na sekta zinazohusiana na shughuli za uchimbaji.

Hayo yamesemwa Mkoani Geita na Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti alipozungumza na wanahabari ambapo amesema kuwa maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini, yakiongozwa na kaulimbiu “Madini ni Utalii, Tuwajibike”, yenye msisitizo wa kuongeza uelewa na mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Mnyeti amesema maonesho hayo ni fursa kwa wadau kuonesha teknolojia zinazotumika katika sekta ya madini, kubadilishana uzoefu na kujadili fursa pamoja na changamoto zinazokabili shughuli za uchimbaji, uchakataji na biashara ya madini.

Aidha Dhamira ya maonesho hayo ni kuiwezesha Tanzania kuwa na maonesho bora yanayohusisha teknolojia za madini na sekta zinazohusiana na madini barani Afrika ifikapo mwaka 2035.

Katika kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia katika uchimbaji na uchakataji wa madini, pamoja na kuwaunganisha wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa teknolojia na wachimbaji, wachakataji na wafanyabiashara wa madini.

Vilevile kupitia maonesho hayo yanalenga kuwaunganisha wachimbaji na taasisi za Serikali, Wizara, taasisi wezeshi, mamlaka za udhibiti pamoja na wadau wa uhifadhi wa mazingira.

Sanjari na hayo hatua hiyo itatoa fursa kwa wadau kukutana, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazojitokeza katika shughuli za madini, huku wakitafuta njia za kuimarisha sekta hiyo.

"Mnyeti amesema ushiriki wa sekta hizo ni muhimu katika kuonesha namna shughuli za madini zinavyoweza kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya Taifa." Amesema mnyeti"

Nitoe Wito Kwa Wananchi watumie fursa hiyo kutembelea maonesho hayo ili kujifunza kuhusu teknolojia, huduma, bidhaa na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo wa thamani wa madini.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com