Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA AWAHAKIKISHIA WANANACHI UPATIKANAJI HUDUMA YA UMEME NGAZI YA VITONGOJI, ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI



Na Marco Maduhu, Elizabeth Cosmas, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, ameelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025-2030, juu ya usambazaji wa huduma ya umeme ngazi ya vitongoji, akieleza kuwa hadi kufikia mwaka huo vitongoji vyote vitakuwa vimepata huduma hiyo.

TAZAMA VIDEO👇👇


Amebainisha hayo leo Septemba 24, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasingili Kata ya Ilola, na Kijiji cha Nyika Kata ya Imesela kwa nyakati tofauti, kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kijiji kwa kijiji.
Amesema, katika utekelezaji wa usambazaji wa huduma hiyo ya umeme ngazi ya vitongoji katika Jimbo la Itwangi, wamepata vitongoji 58 vitakavyonufaika, ambapo katika Kijiji cha Kasingili vitongoji viwili vitapata umeme huo wa REA.

Amevitaja vitongoji hivyo, kuwa ni Ukulikilo chenye kaya 137 na Igenge chenye kaya 135.
Aidha, akiwa katika Kijiji cha Nyika, amesema vitongoji vitatu vitapata huduma hiyo ya kusambaziwa umeme, ambavyo ni Mwalubila kaya 80, Mwalumi kaya 77, na Nhobola kaya 72.

Ametoa rai kwa wenyeviti wa Vitongoji, kutoa ushirikiano pale wataalamu wa REA wanapowawasili, ili kuhakikisha kaya zote zinapata huduma ya umeme, huku akiwasihi wananchi kuweka mifumo ya umeme katika nyumba zao.
Katika hatua nyingine, amesema Kata ya Imesela itapata huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria kwa vijiji vyote, na tayari ujenzi wa tangi umeanza.

Amesisitiza kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hapendi kuona wanawake wakiteseka kwa kufuata maji umbali mrefu, ndiyo maana akatoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

Nao watendaji wa vijiji hivyo viwili, kwa nyakati tofauti wakisoma taarifa zao kwa Mbunge huyo, wamesema kazi ya kusambaza nguzo za umeme katika vitongoji hivyo inaendelea.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, yupo katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji, kwa lengo la kutoa shukrani pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Diwani wa Imesela Seth Msangwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Shinyanga akizungumza.
Diwani wa Ilola Kisena Fred Kisena akizungumza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com