Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA AAHIDI KUTOA MIFUKO YA SARUJI, MABATI NA MBAO UKAMILISHAJI NYUMBA ZA WATUMISHI NGOKOLO NA IGEMBYA ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI

 


Na Marco Maduhu, Elizabeth Cosmas, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, ameahidi kutoa mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kuanzishwa kwa ujenzi wa nyumba ya Mganga katika Zahanati ya Ngokolo Kata ya Tinde, wilayani Shinyanga, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya muda wote, hasa kwa wagonjwa wa dharura nyakati za usiku.

TAZAMA VIDEO👇👇


Pia, ameahidi pia kutoa bati 46, mbao 50 na mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Itubanilo Kijiji cha Igembya ambayo ipo katika hatua ya ukamilishaji.
Ahadi hizo amezitoa leo Septemba 23, 2026, kwa nyakati tofauti wakati, alipofanya ziara katika vijiji vya Ngokolo na Igembya, kwa ajili ya kuwashukuru wananchi, pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Akiwa katika kijiji cha Ngokolo, amesema baada ya kupata taarifa katika mkutano huo kuwa Zahanati ya kijiji hicho haina nyumba ya Mganga, na wananchi wamekuwa wakipata shida ya kupata matibabu hasa nyakati za usiku kwa wagonjwa wenye hali za dharura, ndipo akaguswa na kuamua kuwaunga mkono, na kuahidi kutoa mifuko 150 ya saruji ili ujenzi wa nyumba hiyo uanze mara moja.
“Mbunge wenu katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Zahanati ya Ngokolo nitachangia mifuko 150 ya saruji, na kwa vile na nyie mlianza kuchangia Sh 5,000 kwa kila kaya, endeleeni na mkiwa tayari kuanza ujenzi huo, niambieni ili niilete mifuko hiyo na ujenzi uanze,” amesema Azza.

Aidha, akiwa katika Kijiji cha Igembya Kata ya Nyida, ameahidi pia kutoa mabati 46, mbao 50 na mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Itubanilo, ambayo ipo katika hatua ya ukamilishaji.
Katika mikutano hiyo, Mbunge Azza ametoa pia elimu kwa wananchi kuhusu kuchukua tahadhari za kukabiliana na mvua za El Niño, ambazo zinatarajiwa kuanza kunyesha hivi karibuni.

TAZAMA PICHA 👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com