Serikali imesema imeokoa jumla ya wahanga 160 wa Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambapo Wahanga 126 waliokolewa hapa nchini kabla ya kusafirishwa na wahanga 34 wakirudishwa kutoka nje ya nchi huku Serikali ya Tanzania ikiungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu yenye Kauli Mbiu inayosema “Jihadhari na Utumwa Kupitia Utapeli Mitandaoni”.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi akitoa tamko katika Siku ya Kimataifa ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambapo watuhumiwa 57 wamekamatwa kati yao 45 wamefikishwa mahakamani na watuhumiwa 12 upelelezi unaendelea.
Mhanga Anifa Sylvester(SIO JINA HALISI)akitoa ushuhuda jinsi alivyosafirishwa Kwenda nchini Oman huku Afisa na Wakili wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Chris Mollel akieleza adhabu za kosa hilo la Usafirishaji Haramu wa Binadamu.

Social Plugin