Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA AKAMILISHA HATUA YA UPAUAJI, SASA AIBEBA AJENDA YA KUKAMILISHA ZAHANATI YA SHABULUBA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad (katikati), akiwa ameambatana na wananchi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga,leo Agosti 6, 2026 baada ya kutoa vifaa vya upauaji vilivyowezesha jengo hilo kupata paa. 
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, leo Agosti 6, 2026 wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero, maoni na mapendekezo yao. 
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, leo Agosti 6, 2026 wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero, maoni na mapendekezo yao.  Picha na Kadama Malunde - Shinyanga

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, amesema ataendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, ili wananchi waanze kupata huduma za afya karibu na makazi yao.

Azza ametoa kauli hiyo leo Agosti 6, 2026, wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Shabuluba, ambapo pia amekagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo na kujionea jengo likiwa tayari limepauliwa.

Alisema zahanati hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu alipokuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, lakini baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Itwangi, hakusubiri fedha za Serikali bali aliamua kutumia fedha zake binafsi kuhakikisha hatua ya upauji wa jengo hilo inakamilika.

"Baada ya kunipatia ridhaa ya kuwa Mbunge wenu, nilisema siwezi kusubiri fedha za Serikali. Nikaamua binafsi kuhakikisha jengo hili linapauliwa. Nilifika hapa tarehe 20 Julai, nikakabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya upauaji kwa serikali ya kijiji, na leo nimefurahi kuona jengo limepauliwa na linapendeza," alisema Azza.
Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga.

Amesema hatua iliyobaki sasa ni kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na kuanza kutoa huduma, akiahidi kuendelea kuisemea na kuifuatilia katika mamlaka mbalimbali ili kupata fedha za kuikamilisha.

"Nimepokea ombi lenu la kuendelea kuwashika mkono. Nawahakikishia suala hili ninalibeba. Ndani ya kipindi cha miaka mitano nitahakikisha zahanati hii inakamilika na inaanza kutoa huduma kwa wananchi wa Shabuluba," amesema.

Mbunge huyo amesema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika kuboresha huduma za afya hususan za mama na mtoto, hivyo anaamini Zahanati ya Shabuluba itapata fursa ya kukamilishwa.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad.

"Rais wetu ni Mama mwenye upendo na anayejali afya za wananchi, hasa huduma za mama na mtoto. Nami kama Mbunge wenu nitaendelea kupigania zahanati hii ikamilike ili wananchi wasipate shida kufuata huduma mbali na makazi yao," amesema.

Azza ameongeza kuwa ataendelea pia kushughulikia changamoto nyingine zinazowakabili wananchi wa eneo hilo, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama kupitia mradi wa tanki la maji la Buchama pamoja na kuendelea kuomba Serikali kujenga vituo vipya vya afya katika maeneo ya Usule na Didia ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Aidha, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka maendeleo vijijini, akitolea mfano utekelezaji wa mradi wa umeme katika Kitongoji cha Makengela ambapo kaya 115 zinatarajiwa kunufaika na huduma hiyo.

Mtendaji wa Kijiji cha Shabuluba, Paul Samson, amesema wananchi walijenga zahanati hiyo kwa nguvu zao tangu mwaka 2002 na ilibaki katika hatua ya boma kwa muda mrefu, lakini ndani ya kipindi kifupi tangu Azza achaguliwe kuwa Mbunge, ameonyesha dhamira ya kweli kwa kuchangia fedha zake na kuhakikisha jengo linapauliwa.

Diwani wa Kata ya Usanda, Hamis Gege.

Naye Diwani wa Kata ya Usanda, Hamis Gege, amempongeza Mbunge Azza kwa kugusa maisha ya wananchi wa Shabuluba kwa vitendo, akisema hatua ya kulipatia jengo hilo paa ni mwanzo mzuri wa safari ya kulikamilisha.

Kwa upande wao, wananchi wakiongozwa na Ester Masele wamemshukuru Mbunge huyo kwa kugharamia upauaji wa jengo la zahanati hiyo, wakisema hatua hiyo imewapa matumaini makubwa ya kuona mradi huo unakamilika na kuanza kutoa huduma za matibabu.

Katika mkutano huo, wananchi pia wamewasilisha kero mbalimbali zinazohusu ubovu wa miundombinu ya barabara, upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na uharibifu wa bwawa la umwagiliaji, huku Mbunge Azza akiahidi kuzifuatilia na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Serikali.

TAZAMA VIDEO👇👇

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad (katikati), akiwa ameambatana na wananchi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, leo Agosti 6, 2026. Jengo hilo limepata paa baada ya Mbunge huyo kutoa vifaa vya upauaji, huku akiahidi kuendelea kusimamia na kufuatilia ukamilishaji wa zahanati hiyo ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad (katikati), akiwa ameambatana na wananchi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, baada ya kutoa vifaa vya upauaji vilivyowezesha jengo hilo kupata paa.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad (katikati), akiwa ameambatana na wananchi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, baada ya kutoa vifaa vya upauji vilivyowezesha jengo hilo kupata paa. 
Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, baada ya kupata paa kufuatia vifaa vya upauaji vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad. 
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shabuluba, Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero, maoni na mapendekezo yao. 

Diwani wa Kata ya Usanda, Hamis Gege, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shabuluba wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad. 
Mtendaji wa Kijiji cha Shabuluba, Paul Samson, akisoma taarifa ya kijiji wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com