Meneja wa kanda ya Ziwa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Fredy Kandonga, akizungumza kwenye semina hiyo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo.
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa UCSAF Celina Mwakabwale, akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.

Na Mwandishi wetu
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeongeza kasi ya huduma ya intaneti Kanda ya Ziwa baada ya kubadilisha minara 431 kutoka teknolojia ya 2G kwenda 3G/4G, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma za intaneti zenye ubora zaidi na kuwaletea maendeleo.
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa UCSAF, Fredy Kandonga, amesema hayo Agosti 10, 2026 wakati wa semina ya Wahariri na Wakuu wa Kanda wa vyombo vya habari mkoani Mwanza, akisema maboresho hayo yanalenga kuhakikisha wananchi, hasa wa maeneo ya vijijini na pembezoni, wanapata fursa zaidi za kutumia teknolojia ya kidijitali katika shunguli zao za kila siku.
Kwa mujibu wa Kandonga, upatikanaji wa huduma ya 4G unatarajiwa kuwasaidia wananchi kutumia intaneti kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo elimu mtandao, afya mtandao, biashara mtandao na huduma za kifedha kupitia simu.
Hali hiyo inatarajiwa kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi wanaotegemea huduma za mawasiliano katika shughuli zao za kila siku, huku wafanyabiashara wadogo wakipata fursa ya kutumia majukwaa ya kidijitali kutangaza na kufanya biashara, wanafunzi kupata nyenzo za kujifunzia mtandaoni na wananchi kupata huduma mbalimbali zinazotolewa kwa njia ya kidijitali.
Kandonga amesema Serikali imetumia ruzuku ya takribani Sh9.14 bilioni katika utekelezaji wa mradi huo wa kuboresha uwezo wa minara.
Mbali na kuboresha minara iliyopo, amesema UCSAF inaendelea na ujenzi wa minara mipya 287 katika Awamu ya 10 ya Mradi wa Mawasiliano, ambapo wananchi takribani milioni 2.9 wanatarajiwa kunufaika.
Mradi huo unatekelezwa katika kata 287 zenye vijiji 359 na unagharimu takribani Sh29 bilioni za ruzuku ya Serikali, huku ukitarajiwa kukamilika Machi 2027.
Kanda ya Ziwa imepangiwa minara 67 katika mikoa sita, ambapo Mwanza inaongoza kwa kuwa na minara 21, ikifuatiwa na Kagera 14, Mara 11, Simiyu minane, Geita saba na Shinyanga sita.
Kandonga amesema hadi sasa minara saba imewashwa na wananchi tayari wanapata huduma kupitia minara hiyo.
Amesema hatua hizo ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia UCSAF kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano bila kujali wanapoishi, hali ya uchumi au hali ya kijamii.
“Lengo la Serikali kupitia UCSAF ni kuwaunganisha wananchi wa pembezoni, hasa vijijini, na huduma za simu, intaneti, utangazaji na posta,” amesema.
Amesema hadi Aprili 2026, huduma ilikuwa imekamilika katika kata 2,012 zenye vijiji 5,132, huku wakazi takribani 29,721,003 wakipata huduma kupitia minara 2,158.
Kandonga amesema Kanda ya Ziwa pekee imejengewa takribani minara 414 katika kata zipatazo 380 za Mwanza, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera.
Kwa upande wake, Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa UCSAF, Celina Mwakabwale, amewataka wahariri kuzingatia misingi ya uandishi wa habari pamoja na kuimarisha uhusiano na taasisi hiyo ili kupata taarifa sahihi kuhusu shughuli na mipango yake.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko, meishukuru UCSAF kwa kuwaandalia wahariri semina hiyo, akisema imewapa uelewa zaidi kuhusu majukumu na kazi za taasisi hiyo.
Soko amesema uelewa huo ni chachu kwa wahariri kuandika taarifa zinazoeleza uhalisia, umuhimu na utekelezaji wa mipango ya UCSAF, hususan katika juhudi za kupunguza umaskini.
Amesema mawasiliano yana nafasi kubwa katika kukuza shughuli za kiuchumi, hivyo uwekezaji katika miundombinu na huduma za mawasiliano unaweza kuwa kichocheo cha maendeleo ya wananchi.
Amesisitiza kuwa mawasiliano siyo suala la kuwasiliana pekee, bali ni sehemu ya uchumi kwa kuwa yanawezesha wananchi kupata taarifa, kufanya biashara, kupata huduma za kifedha na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia teknolojia ya kidijitali.

Social Plugin