Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna wimbi la kuwashawishi vijana, hususan katika mataifa ya Afrika, kugeuka dhidi ya mataifa yao, akieleza kuwa hali hiyo inalenga kudhoofisha nchi zinazoendelea.
Mkuu huyo wa nchi amesema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akifungua mkutano wa Chama cha Mawakili Tanzania jijini Arusha.
“Tunashuhudia mataifa yakihujumiana, tunashuhudia vijana kulaghaiwa na kumezeshwa sumu dhidi ya mataifa yao kushawishiwa kuhujumu chumi zao zilizojengwa kwa nguvu kubwa,”
“Jinsi nchi zetu zinazoendelea tunavyokwenda mbele wengine wanaangalia njia na mbinu za kutuvuta nyuma tusiende na kasi ile tunayokusudia,” amesema.


Social Plugin