Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA IMEJENGA MISINGI IMARA YA HAKI ZA BINADAMU


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofuata na kulinda haki za binadamu, akisisitiza kuwa serikali imeweka mifumo mbalimbali ya kisheria inayolenga kuhakikisha haki hizo zinatekelezwa na kulindwa.

Akizungumza leo Julai 13, 2026, wakati akifungua mkutano wa Chama cha Mawakili Tanzania jijini Arusha, Rais Samia amesema Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikizingatia masuala ya haki za binadamu.

“Mtakumbuka kwamba sisi Tanzania tuliweka kwa mara ya kwanza kwenye katiba yetu mwaka 1984 mtiririko wa haki za binadamu na tukatanua wigo wa haki hizo,” amesema Rais Samia.

Amesema pamoja na hatua hiyo, serikali imetunga sheria mbalimbali zinazolenga kulinda na kuimarisha utekelezaji wa haki za binadamu nchini.

“Pamoja na hayo tumetunga sheria nyingine nyingi ambazo zinakwenda kulinda na kuweka nguvu utekelezaji wa haki hizo za binadamu. Tumetoa nafasi kwa wananchi wetu wanapohisi haki zao za binadamu zinavunjwa watumie mahakama kwenda kudai au kutetea haki yao,” amesema.









Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com