Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA MADINI YAFUNGUA USAJILI WA MKUTANO WA TANZANIA MINING AND INVESTMENT CONFERENCE (TMIC) 2026

 Wizara ya Madini imefungua rasmi usajili kwa wadau wanaotaka kushiriki Mkutano wa Tanzania Mining and Investment Conference (TMIC) 2026, utakaofanyika kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre – JNIC) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa kimataifa unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini, wakiwemo wawekezaji, wachimbaji, wafanyabiashara, taasisi za fedha, wataalamu, watunga sera na washirika wa maendeleo kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji, kuimarisha ushirikiano na kuendeleza ukuaji wa sekta ya madini nchini.

TMIC 2026 utaongozwa na kaulimbiu isemayo "Madini Yaliyoongezwa Thamani: Chachu ya Ukuaji wa Viwanda na Uchumi" (Value-Added Minerals: The Engine of Industrialization and Economic Growth), ikisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya madini ili kuchochea maendeleo ya viwanda, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Taifa.

Wizara ya Madini imewahimiza wadau wote wa sekta hiyo pamoja na wananchi wenye nia ya kushiriki mkutano huo kujisajili mapema kupitia tovuti ya conference.madini.go.tz au kwa kuskani Msimbo wa Haraka (QR Code) uliowekwa kwenye tangazo rasmi la usajili.

TMIC 2026 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuonesha fursa zilizopo katika sekta ya madini nchini Tanzania, kuvutia uwekezaji, kubadilishana uzoefu na teknolojia, pamoja na kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com