Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA MSUMBIJI ZATIA NGUVU USHIRIKIANO WA KIUSALAMA MIPAKANI.

Mwandamizi wa Polisi SACP Marco  G Chilya akizungumza katika mkutano wa Ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika leo tarehe 23 juni 2026 ukumbi wa Heritage Cottage Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma 
Kamanda wa Jimbo la Niasa nchini Msumbiji Celestino Albano Vianeque akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza katika ukumbi wa Heritage Cottage katika mkutano uliowakutanisha baina ya nchi mbili Tanzania na Msumbiji kama ishara ya ujirani mwema kati ya nchi hizo mbili.


Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma. 


Mkuu wa wilaya ya Nyasa Mhe. Perres Magiri, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma, amefungua rasmi mkutano wa ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. 


Mkutano huo wa siku mbili ambao umeanza  kufanyika leo Juni 23 hadi 24, 2026, umewakutanisha viongozi na maafisa kutoka taasisi mbalimbali za usalama za nchi hizo mbili kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiusalama.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mhe. Magiri amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Msumbiji ili kudumisha amani, usalama na utulivu katika maeneo ya mipakani. 


Ameeleza kuwa mikutano ya aina hiyo imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kujenga mahusiano mazuri, kuimarisha mawasiliano na kutafuta suluhisho la pamoja kwa changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoweza kujitokeza.


Katika mkutano huo, washiriki wanatarajia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo udhibiti wa uhalifu wa kuvuka mipaka, usimamizi wa mipaka na mbinu za kuendeleza ushirikiano wa kiutendaji kati ya vyombo vya usalama vya Tanzania na Msumbiji. 


Aidha, mkutano huo unalenga kubadilishana uzoefu na mbinu bora za utekelezaji wa majukumu ya kiusalama kwa manufaa ya wananchi na mataifa yote mawili.


Awali kabla ya kuanza kwa kikao kazi hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi 


Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amepata fursa ya kumtambulisha Kamanda wa Jimbo la Niasa nchini Msumbiji, Kamishna Msaidizi wa Polisi Celestino Albano Vianeque, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa vyombo vya usalama vya nchi hizo mbili.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com