Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Group, Renatus Kiluvia, akizungumza wakati wa kutambulisha NANDY FESTIVAL 2026 Shinyanga.
Kuelekea uzinduzi wa NANDY FESTIVAL 2026 na miaka 10 ya muziki wa msanii Nandy, waendesha daladala za baiskeli Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa pampu za baiskeli kama sehemu ya kutambua mchango wao katika huduma ya usafiri kwa wananchi.
Akizungumza wakati akigawa pampu za baiskeli bure kwa waendesha daladala za baiskeli, Mwakilishi wa NANDY FESTIVAL 2026, Remmy Nguvu, amesema waendesha daladala za baiskeli ni miongoni mwa wadau muhimu wanaosaidia wananchi kufika maeneo mbalimbali kwa gharama nafuu, hivyo wameona ni muhimu kuwapongeza kwa mchango wao kupitia zawadi hiyo.
Amesema shughuli hiyo ni sehemu ya maandalizi ya NANDY FESTIVAL 2026, tamasha litakalokwenda sambamba na kusherehekea miaka kumi ya safari ya muziki wa Nandy, huku likitarajiwa kuwakutanisha maelfu ya mashabiki wa muziki kutoka maeneo mbalimbali.
Ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Shycom Juni 20, 2026 kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali watakaopanda jukwaani, akiwemo Bilinass, Lina, Rayvanny pamoja na wengine wengi.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Group, Renatus Kiluvia, amesema hatua ya kuwapatia pampu waendesha dala dala za baiskeli inaonyesha namna NANDY FESTIVAL 2026 inavyothamini mchango wa makundi mbalimbali ya kijamii yanayowahudumia wananchi kila siku.
Ameeleza kuwa waendesha baiskeli hao wamekuwa na nafasi kubwa katika kurahisisha usafiri wa abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine, jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wengi wa Manispaa ya Shinyanga.Tamasha la NANDY FESTIVAL 2026 linatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa ya burudani mwaka huu Mkoani Shinyanga, likiwa na lengo la kuwaleta pamoja mashabiki wa muziki
Social Plugin