Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS yawakaribisha wadau VIWANGO MARATHON


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa mbio za marathon zijulikanazo kama ‘Viwango Marathon’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, huku likihamasisha matumizi ya bidhaa zilizothibitishwa na TBS pamoja na kuimarisha afya kwa jamii kupitia michezo.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Mei 23, 2026 katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18, 2026 jijini Dar es Salaam, Afisa Ukaguzi wa TBS, Mhandisi Nyabuchwenza Methusela amesema marathon hiyo pia inalenga kurejesha kwa jamii kupitia utoaji wa vifaa mbalimbali katika hospitali zenye uhitaji kwa kushirikiana na wadhamini pamoja na washiriki wa mbio hizo.

“Mbali na kukimbia, hili ni tukio la kijamii linalolenga kuhamasisha matumizi ya bidhaa zilizothibitishwa na TBS, kuhamasisha Viwango lakini pia kurudisha kwa jamii kupitia utoaji wa msaada katika hospitali zinazohitaji,” amesema Mhandisi Nyabuchwenza .

Aidha, amewakaribisha wananchi, wadau wa michezo na taasisi mbalimbali kushiriki katika mbio hizo kwa kujisajili kwa gharama ya shilingi 30,000 kwa kila mshiriki.

Kwa upande wake, Afisa Ukaguzi wa TBS, Mhandisi Hassani Zaidi Amiri amesema marathon hiyo itakuwa na mbio za kilometa tano, kilometa 10 pamoja na kilometa 21, hatua inayolenga kutoa fursa kwa washiriki wa makundi mbalimbali kushiriki kulingana na uwezo wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com