Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MBUNGE AZZA HILLAL ATANGAZA MAKAO MAKUU YA OFISI YA MBUNGE ITWANGI, AAHIDI KUKAMILISHA UJENZI SHULE YA SEKONDARI NHUMBILI

Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad akipiga magoti mbele ya wananchi wa Kijiji cha Itwangi, Kata ya Itwangi, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini, kuwashukuru kwa imani waliyoionesha kwa kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. — Picha na Kadama Malunde
Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itwangi kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Bw. Said Nassoro (katikati) akiwa amekaa na wananchi wakati Mhe. Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itwangi kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Erenestina Richard akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itwangi kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Itwangi Mhe. Lydia Pius akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itwangi kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari Nhumbili katika kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari Nhumbili katika kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Tinde Mhe. Japhari Kanolo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad ametangaza rasmi kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Itwangi yatakuwa katika Kijiji cha Itwangi Kata ya Itwangi, huku akiahidi kusimamia kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nhumbili iliyopo Kata ya Tinde ili kuboresha huduma za elimu kwa wananchi wa jimbo hilo.

Mhe. Azza ametoa kauli hiyo leo Mei 17, 2026 wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa Kijiji cha Itwangi na Nhumbili kwa kuchagua CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo wananchi walimchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Itwangi pamoja na kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo jipya la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Itwangi, Mhe. Azza amesema lengo la kuweka Makao Makuu ya Ofisi ya Mbunge katika kijiji hicho ni kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze kupata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao kwa urahisi.

Amesema tayari serikali ya kijiji imetoa chumba kwa ajili ya shughuli za ofisi hiyo ambapo kila wiki kutakuwa na siku  mbili maalumu za mbunge kukutana na wananchi wa Jimbo la Itwangi.

“Makao Makuu ya Ofisi ya Mbunge yatakuwa hapa kijiji cha Itwangi Itwangi. Nitakuwepo hapa nikisaidiwa na Katibu wangu Said Nassoro ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa karibu zaidi,” amesema Azza.

Katika hatua nyingine, akiwa katika Kijiji cha Nhumbili Kata ya Tinde, Mbunge huyo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Nhumbili iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 17 hadi kufikia hatua ya renta.

Amesema ameridhishwa na jitihada za wananchi wa kijiji hicho waliofanikiwa kujenga majengo mawili yaliyofikia hatua ya upauaji, huku akiwapongeza kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo ya elimu.

“Mimi kama Mbunge wenu nalibeba suala la ujenzi wa Shule ya Sekondari Nhumbili. Nitahakikisha shule hii inakamilika ili watoto wetu wapate mazingira bora ya kujifunzia,” amesema Mhe. Azza.
Mbunge Azza pia amewahakikishia wananchi kuwa serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Itwangi ikiwemo mradi wa maji ya Ziwa Victoria kwa maeneo ya Nhumbili na Ngokolo ambapo serikali imetenga shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kufikisha huduma hiyo.

Aidha amesema serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Nsalala – Butini pamoja na barabara ya Itwangi – Mwakasongwe na barabara ya Usule – Buchama – Tinde ambapo tayari shughuli za ujenzi zimeanza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Erenestina Richard. 

Katika ziara hiyo, Mbunge huyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Erenestina Richard  ambaye amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuiamini CCM kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Katibu huyo amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaletea maendeleo wananchi kupitia maboresho ya huduma za maji, afya, elimu, umeme pamoja na miundombinu ya barabara.

Wananchi wa maeneo hayo wamempongeza Mbunge huyo kwa kuanza ziara ya kuwashukuru wananchi pamoja na kueleza mipango ya maendeleo ya jimbo hilo, wakisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa karibu zaidi.



@malundeblog

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad amekagua ujenzi wa shule Mpya ya Nhumbili iliyopo katika kata ya Tinde Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

♬ original sound - Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com