Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAGAMBO AGUSA SEKTA YA ELIMU NYAMATARE,AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA KUJENGA VYUMBA VITANO VYA MADARASA

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Fortunatus Magambo ameandika historia mpya katika Kata ya Nyamatare baada ya kujitolea kujenga vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Msingi Ring’wani, hatua inayotajwa kuwa mkombozi kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Bw. Magambo alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea shule hiyo mwaka 2024 na kushuhudia hali ya uchakavu wa miundombinu pamoja na upungufu mkubwa wa madarasa uliokuwa ukiathiri mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

“Nilipofika hapa niliguswa kuona watoto wakisomea katika mazingira magumu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. Nimeamua kushiriki kuboresha mazingira haya ili watoto wetu wapate sehemu bora ya kujifunzia,” amesema Bw. Magambo.

Tayari kazi ya uchimbaji wa msingi pamoja na hatua za awali za ujenzi wa vyumba hivyo vitano imeanza, huku lengo likiwa ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya Julai 2026 kuisha.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nyamatare, Mgaya Maheke amemshukuru Bw. Magambo kwa moyo wake wa kujitoa kusaidia maendeleo ya elimu katika kata hiyo.

“Tunawapongeza wadau wetu wa maendeleo wanaoendelea kushirikiana nasi kuinua sekta mbalimbali za kijamii. Ushirikiano huu ni faraja kubwa kwa wananchi wetu,” amesema Mheshimiwa Maheke.

Ameongeza kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wote wanaojitokeza kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kutokana na Elimu kuwa nguzo muhimu katika jamii na ndio ufunguo wa maisha, jamii imeendelee kuhimizwa kuleta maendeleo katika maeneo yao wao wenyewe na siyo tu kuiachia serikali peke yake.












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com