Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMISHNA WA POLISI JAMII AFANYA ZIARA KAGERA, AHIMIZA AMANI

Mkurugenzi wa taasisi ya mabalozi  wa amani PPAT  Maulid Rashidi Kambuga akitoa taarifa ya taasisi.


Na Theophilida Felician -  Kagera

Kamishna wa polisi nchini CP Alex Mkama amefanya ziara ya kujitambulisha mkoa Kagera ambapo amehimiza masuala  mbalimbali katika kuudhibiti uhalifu.

Kamishna Mkama akiwa kwenye kikao cha wadau wa usalama kilichofanyika manispaa ya Bukoba amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya maboresho makubwa ya mifumo yake ikilenga kuwashirikisha wananchi jambo litakalo saidia kuutokomeza uhalifu na wahalifu kwa ujumla.

Amefafanua kwamba lengo la jeshi hilo nikuhakikisha amani  inadumu nyakati zote hivyo niwajibu wa kila mwananchi kushiriki ipasavyo na kuitunza kwa nguvu zote.

Amewapongeza wananchi mkoa Kagera kuwa watulivu hususani kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 hivyo amewahakikishia kwamba jeshi hilo linaendelea kushirikiana nao  kwa ukaribu zaidi.

Mkurungezi wa taasisi ya mabalozi wa amani Mhe. Mauldi Rashidi Kambuga ameelezea namna taasisi hiyo ilivyojikita kuhamasisha amani kwa jamii hususani kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025  taasisi ilisimama katika majukwaa na kutoa elimu hatimaye mkoa ulisalia katika hali ya  utulivu.

Amelishukuru jeshi la polisi kwa namna linavyotoa ushirikiano kwa taasisi hiyo hivyo amemuomba kamishna Alex kufikisha salamu za PPAT kwa mkuu wajeshi la polisi nchini huku akiliomba ushirikiano wa kupatiwa vibali vya kutoa elimu ya amani nchi nzima.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa kimila,wenyeviti wa mitaa, watendaji kata, wawakilishi wa tiba asili, kampuni za ulinzi na askari polisi.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com