Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TPDC YAONGOZA UCHIMBAJI WA GESI SONGO SONGO, SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO YA KUONGEZA LESENI YA PAET


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Kitalu cha Gesi Asilia cha Songo Songo kina jumla ya visima 12, ambapo Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imechimba visima tisa, huku Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAET) ikichimba visima vitatu.

Mhe. Makamba amesema hayo leo Mei 12, 2026, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini, Mhe. Hasnain Gulamabbas Dewji, katika Mkutano wa Tatu, Kikao cha 27 cha Bunge la 13 mjini Dodoma, aliyehoji idadi ya visima vya gesi asilia vilivyochimbwa hadi sasa katika Kisiwa cha Songo Songo.

Amesema kuwa Kitalu cha Songo Songo kinaendelea kuzalisha wastani wa futi za ujazo milioni 84.7 za gesi asilia kwa siku, kulingana na mahitaji yaliyopo.

Aidha, Mhe. Makamba amesema kuwa kutokana na leseni ya sasa ya uendelezaji wa gesi asilia kufikia ukomo mwezi Oktoba 2026, timu ya majadiliano ya Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni ya PAET kuhusu uwezekano wa kuongeza muda wa leseni hiyo ili kuendelea na shughuli za uzalishaji katika kitalu hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com