Kikao cha Baraza la Madiwani la robo ya tatu la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kimepitisha maazimio kadhaa muhimu yanayolenga kuboresha sekta ya elimu, ukusanyaji mapato pamoja na usalama wa jamii.
Akizungumza katika kikao hicho chenye lengo la kupokea na kujadili taarifa za maendeleo kwa kipindi cha robo hiyo (Januari-Machi) mwaka wa fedha 2025/2026 Aprili 24,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Josephat Limbe, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha kwa wakati miradi ya maendeleo hususan katika sekta ya elimu.
"Baraza limeelekeza kuwa Mkurugenzi na menejimenti yako miradi yote ya elimu ikamilike ifikapo Mei 25,2026 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Sera ya Elimu ya mwaka 2023 inayolenga kuboresha mfumo wa elimu, ikiwemo wanafunzi wa madarasa ya tano na sita kuhitimu pamoja ifikapo mwaka 2027, pamoja na mabadiliko ya muundo wa elimu ya msingi na sekondari" ameongeza Mhe. Limbe.
Katika suala la mapato, Baraza limeagiza kuwa ifikapo Juni 30, Halmashauri iwe imefikia lengo la asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Aidha, Halmashauri imetakiwa kuchunguza na kufuatilia riba zinazotozwa na taasisi za huduma ndogo za kifedha (Microfinance) ili kuhakikisha zinazingatia sheria ya fedha na kuwa rafiki kwa wananchi.
Sambamba na hayo, Baraza hilo limepitisha azimio la kuanzisha kamati maalum ya kudhibiti utoro na mimba kwa wanafunzi, hatua inayolenga kuinua kiwango cha elimu katika Halmashauri hiyo.
Baada ya maamuzi ya Baraza, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo, Fabiani Makongo na Afisa usafirishaji Wilayani humo Ezra Leonard, wamepongeza juhudi za madiwani kwa kusimama kidete kutetea masilahi ya wananchi, hususani wajasiriamali wadogo, wakisema hatua hiyo inaleta matumaini mapya na kuongeza imani ya wananchi kwa viongozi wao.
Makongo ameeleza kuwa msimamo huo wa madiwani unachochea ari ya wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya eneo lao, huku akibainisha kuwa ulinzi wa masilahi ya wajasiriamali ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa ndani.
Nae Ezra Leonard Amesisitiza kuwa uongozi unaojali na kusikiliza wananchi ni chachu ya maendeleo endelevu, na kwamba juhudi hizo zinapaswa kuendelezwa ili kujenga jamii yenye ustawi, mshikamano na fursa sawa kwa wote.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter N. Masindi akizungumza kwenye kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani kikilenga kupokea na kujadili taarifa za maendeleo kwa kipindi cha robo hiyo Januari-Machi mwaka wa fedha 2025/2026 Aprili 24,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mwakilishi wa Katibu Tawala mkoani Shinyanga Baraka Bulongo akizungumza kwenye kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani kikilenga kupokea na kujadili taarifa za maendeleo kwa kipindi cha robo hiyo Januari-Machi mwaka wa fedha 2025/2026 Aprili 24,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enock Reuben akizungumza kwenye kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani kikilenga kupokea na kujadili taarifa za maendeleo kwa kipindi cha robo hiyo Januari-Machi mwaka wa fedha 2025/2026 Aprili 24,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Social Plugin