Na mwandishi wetu
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amesema ameipokea kwa furaha ripoti ya Tume ya Uchunguzi, akieleza kuwa imekuwa chombo muhimu katika kuliponya Taifa kutokana na majeraha ya tukio la Oktoba 29, 2015.
Askofu Shoo amesisitiza kuwa hatua ya tume hiyo kuzungumza ukweli waziwazi pamoja na kutoa mapendekezo ya kina ni msingi imara wa kujenga upya mshikamano wa kitaifa na kurejesha imani kwa wananchi.
Amesema kuwa endapo Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa ndani ya ripoti hiyo, Tanzania itaendelea kudumisha sifa yake ya kuwa kisiwa cha amani barani Afrika.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa dini, ukweli una nguvu ya kuponya na kuunganisha jamii, na ndio sababu ripoti hiyo imekuja kwa wakati sahihi ambapo Taifa linahitaji maridhiano, uwazi na haki.
Aidha, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa, dini na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika kuhakikisha mapendekezo ya tume yanatekelezwa kikamilifu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Amesisitiza kuwa amani ya Taifa siyo jambo la bahati, bali ni matokeo ya maamuzi sahihi, haki na uwajibikaji unaozingatia maslahi mapana ya wananchi wote.

Social Plugin