Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Petro Magoti amepokea tuzo ya shukrani kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa Kuthamini mchango wake mkubwa katika kubaini, Kuzuia na kutanzua uhalifu mkoani humo.Tuzo hiyo imetolewa Aprili 30, 2026 katika sherehe ya siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Pwani iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kibaha.
Mhe Magoti amekuwa msaada mkubwa katika kuhamasisha amani na usalama ndani ya wilaya ya Kisarawe. Aidha aliandaa mafunzo kwa maafisa usafirishaji 800 wa wilaya ya Kisarawe ili kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa kufuata sheria za usalama barabarani.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge alihimiza weledi, utii , haki na aliwataka askari kuwa wepesi kutatua changamoto kwa muda mfupi.
Sherehe hizo ziliambatana na michezo na burudani mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, kukimbiza kuku ambapo askari walicheza pamoja na makundi mbalimbali ya jamii.








Social Plugin