Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHALINZE WAHIMIZWA MAHUSIANO MEMA ILI KUINUA TAALUMA SHULENI

Diwani wa kata ya Bwilingu, halmshauri ya Chalinze, Mh. Lawrence Peter
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibiki, Bi. Hawa Waziri


NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE.

DIWANI wa kata ya Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze, mkoa wa Pwani Mh. Lawrence Peter amewahimiza wazazi kujenga tabia ya kuwa na mahusiano mema na walimu shuleni.

Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha wazazi kilichoitishwa na shule ya Msingi Kibiki kwaajili ya wazazi kupokea taarifa mbalimbali kutoka shuleni hapo jana. 

Mh. Diwani aliiambia hadhira hiyo kuwa walimu wanastahili kupewa sifa na sio kubezwa kwani kati ya wanafunzi 94 waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana, wanafunzi 93 walifaulu na mwanafunzi 1 tu ndiye aliyefanya vibaya na kufanya shule kuingia kwenye kumi bora katika halmashauri hiyo.

"Kwa kweli walimu wetu wanafanya kazi kubwa sana. Na mimi niwaombe wazazi wenzangu tusiwakatishe tamaa, tuwaunge mkono. Haya maneno ambayo tunayoyasikia  mitaani haya naomba yapuuuze. Watavunjika moyo hawa. Sisi tunafikiria kuwahamisha, lakini wao wataanza kuomba kuhama kabla ya sisi kuwahamisha", alisema Mh. Diwani.

Mh. Lawrence ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo ,ameahidi kutoa ushiriakiano wa kutosha shuleni hapo na kuwaomba wazazi kufika ofisini kwake endapo wana jambo ambalo wanahisi hawawezi kumwambia mwalimu mkuu  au mwenyekiti wa kitongoji.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi. Hawa Waziri alianza kumshukuru diwahi huyo kwa kukubali kuwa mlezi wa shule hiyo na kufanikisha kupatikana kwa madawati 20 kutoka katika mfuko wa jimbo na kukubali kulichukua suala la ukarabati wa baadhi ya vyumba vya madarasa shuleni hapo kulipeleka katika ngazi za juu kwa utekelezaji.















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com