Na Mapuli Kitina Misalaba
Zoezi la Samia Ardhi Kliniki limeendelea katika viwanja vya Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga, ambapo huduma mbalimbali za masuala ya ardhi zinatolewa, ikiwemo utoaji wa hati miliki papo kwa papo.
Akizungumza katika eneo la zoezi hilo, Mthamini kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi Mkoa wa Shinyanga, Neema Augustine Mbaga, amesema kliniki hiyo ilianza Machi 2 na itahitimishwa Machi 7, 2026, ikitoa fursa kwa wananchi hususan wanawake kupata huduma za umiliki wa ardhi kwa urahisi.
“Tupo hapa katika viwanja vya Soko Kuu tangu tarehe 2 na tutaendelea hadi tarehe 7. Tunatoa huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa hati miliki papo kwa papo. Wananchi wote wanahudumiwa lakini akina mama wamepewa kipaumbele maalum,” amesema Mbaga.
Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri wa masuala ya ardhi, utatuzi wa migogoro kupitia mabaraza ya ardhi ya wilaya, uthamini wa mali, upimaji na ramani, pamoja na ushauri kuhusu vibali vya ujenzi na mipango miji na kwamba Masaveya pia wanatembelea maeneo yenye changamoto za mipaka kwa ajili ya marekebisho.
Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, amesema tayari baadhi ya wanawake wameandaliwa na kukabidhiwa hati miliki zao huku elimu ya masuala ya ardhi ikiendelea kutolewa kwa wote wanaofika katika kliniki hiyo.
“Wapo wanawake ambao waliomba kumilikishwa ardhi zao, tayari tumewaandalia hati na baadhi yao tumewakabidhi. Tunaendelea kutoa elimu ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria,” amesema Gwaltu.
Afisa Ardhi Mwandamizi Mkoa wa Shinyanga, Halima Mrinji, amesema lengo la zoezi hilo ni kuwainua wanawake kiuchumi kupitia umiliki halali wa ardhi.
Naye Afisa Ardhi Mwandamizi wa Manispaa ya Shinyanga, Lela Amos Chipanyaga, amesema mwitikio ni mkubwa ambapo zaidi ya wanawake 30 walihudumiwa siku ya kwanza na zaidi ya 40 siku ya pili, baadhi wakikabidhiwa hati zao na wengine kuandaliwa malipo ya gharama za umilikishaji.
Baadhi ya wanufaika wa zoezi hilo ni Judiya Kabendela wa Majengo Mapya, Wingwe Yohana mkazi wa Shinyanga na Alistiles Njunwa wa Kata ya Lubaga, ambao wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kumiliki ardhi zao kisheria.
Zoezi hilo linafanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, 2026, chini ya kauli mbiu isemayo: “Mwanamke haki yao milki Ardhi yako sasa.” Mkoa wa Shinyanga utaadhimisha siku hiyo kimkoa katika Halmashauri ya Ushetu.
Wananchi wakipata huduma mbalimbali za ardhi katika Samia Ardhi Kliniki inayoendelea Viwanja vya Soko Kuu Shinyanga.
Maafisa ardhi wakitoa ushauri, upimaji na huduma za uthamini kwa wananchi waliojitokeza katika Samia Ardhi Kliniki.

Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Picha ya pamoja.
Social Plugin