Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MENEJA UWANJA MKWAKWANI ASIMAMISHWA KAZI



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Meneja wa Uwanja wa Mpira wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, Akida Machai, ameondolewa katika nafasi yake kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa uwanja huo. 

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubainika kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika usimamizi wa miundombinu ya uwanja huo.
‎Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abrahman, ameiagiza Kamati ya Siasa ya Mkoa kumsimamisha kazi mara moja Meneja wa Uwanja wa CCM  Mkwakwani Akida Machai kufuatia kubainika kwa mapungufu mbalimbali katika usimamizi wa uwanja huo.
‎Mwenyekiti ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya miundombinu katika Uwanja wa Mkwakwani unaomilikiwa na CCM, kwa lengo la kujionea maendeleo na changamoto zilizopo katika uwanja huo.

"Tulikuweka wewe kama meneja tukiamini utatusaidia kuhakikisha muda wote uwanja umekuwa bora na unaweza kutumika lakini ukija wakati wowote uwanja umekuwa mama mdogo za wanyama haiwezekani mpaka leo hii boti vimeletwa lakini havijafungwa mmeviacha vikaotewa na majani nimekaa tu,  viongozi tuliowateua na kuwachagua ili uwanja huu uwezo kukidhi vigezo mpaka kufikia kati uwanja unafungiwa na TFF hatuwezi kukubali na ninatoa mwezi mmoja kuhakikisha viti vinafungwa kwa haraka "alisisitiza Rajabu.

"Maelekezo ninayotoa Kamati ya siasa kaeni tutafute meneja mwingine atajayesiamamia uwanja huu ili changamoto hizi ziweze kuondoka lakini la pili yule mwenyw baba pale nje ya uwanja ambayo haijakidhi vigezo na TFF walishasema ile baba inazuia mashabiki kuingia ndani ya uwanja kwamba iondoke lakini mpaka leo haijaondolewa sijui kumiliki ana mapembe gani yule ni mpangaji wetu ndani chama cha mapinduzi lakini leo  anakigomea chama leo hii nahitaji baa hii ambayo haijakidhi vigezo iondoke ili maelekezo yaliyotolewa na TFF kwa chama cha mapinduzi tuweze kutekeleza, "alisema Rajab. 

‎Kwa upande wake, aliyekuwa Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani, Akida Machai, amesema changamoto ya uhaba wa nguvu kazi imekuwa sababu ya kushindwa kusimamia ipasavyo zoezi la usafi na matengenezo ya uwanja huo. Ameeleza pia kuwa tayari aliwasilisha taarifa kwa uongozi wa CCM akiomba kupatiwa fedha kwa ajili ya ufungaji wa viti katika majukwaa ya uwanja huo.
‎Uwanja wa CCM Mkwakwani ni miongoni mwa viwanja vikongwe vya soka nchini Tanzania, ukitumika kwa michezo ya ligi na mashindano mbalimbali pamoja na matukio mengine ya kijamii. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni uwanja huo umekuwa ukikumbwa na changamoto ya kufungiwa mara kwa mara na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kutokidhi baadhi ya vigezo vya ubora vinavyotakiwa kwa ajili ya mashindano.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com