Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC KISHAPU - VITENDO VINAVYOKIUKA SHERIA HAVITARUHUSIWA

 
                                     Na Mwandishi wetu

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa majina ya Manjano Mabeshi (50)  Mkazo wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga amepoteza maisha kufuatia tukio la kukatwa na kitu chenye ncha kali.


Akizungumza wakati wa mazishi Machi 5, 2026, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, amewataka wananchi kutojichukulia Sheria mkononi na badala yake kudumisha amani na kuepuka migogoro inayoweza kusababisha vitendo vya ukatili.


"Ninatoa  pole nyingi kwa familia ya marehemu na jamii ya Kijiji cha Mwasubi kwa tukio hili, serikali inawahakikishia kuwa vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa kina ili wote waliohusika kutenda tukio hilo watiwe nguvuni na sheria itafuata mkondo wake" amesema Mhe. Masindi.


Mhe. Masindi amewataka Wananchi kuendelea kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola na amewasihi wananchi kuwa endapo kuna migogoro ama ugomvi kati ya mtu na mtu ama familia na familia wafikishe mashtaka kwenye vyombo husika na watatuliwa kwa mujibu wa sheria.


"Amani na utulivu ni msingi wa maendeleo yetu sote. Tunaomba wananchi kuendelea kudumisha amani na kuepuka migogoro inayoweza kusababisha vitendo vya ukatili wa namna hii. Tunaweza kujenga jamii yenye amani na maendeleo kwa kushirikiana na vyombo vya dola na kufanya kazi kwa bidii". ameongeza


Amewahakikishia Wananchi  wa Mwasubi na Wilaya ya Kishapu kwa Ujumla kuwa serikali iko pamoja nao hivyo wawe tayari kutoa taarifa za uhalifu na waarifu punde wanapoyabaini.


Kwa mujibu wa taarifa, tukio hilo lilitokea Februari 24, 2026 majira ya saa 8 usiku ambapo watu wawili walivamiwa na kushambuliwa ni Manjano Mabeshi  Mwanaume (50) na Suzana Joseph Mwanamke (34), mwanamke ambaye ni mke mdogo wa marehemu.


Manjano Mabeshi alifariki dunia Machi 1, 2026 wakati akiendelea kupatiwa matibabu, huku Suzana Joseph akiripotiwa kuendelea vizuri kiafya na sasa ameruhusiwa na  kurejea nyumbani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com