Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Bara, John Mongella, ameelezea kuridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa wa asilimia 95 katika kituo cha Afya cha Tinde mkoani Shinyanga, huku akiahidi kuchukua changamoto ya upungufu wa majengo ya kutolea huduma, na upungufu wa wahudumu wa afya ili kuzifanyia kazi.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM, Mongella amesema hayo baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa katika kituo cha Afya Tinde pamoja na kuwapatia mahitaji ya kibinadamu.
Nao wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo wamesema wanaridhika na huduma wanazopatiwa huku wakiomba ziboreshwe zaidi ili kukidhi mahitaji ya huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo.
Naye, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya Tinde, Dkt. Evance Munisi, amesema kituo hicho kinahudumia wananchi wengi kwa kuwa kipo njiapanda ya barabara ya Tabora-Shinyanga na Shinyanga-Kahama, ambapo ameomba serikali ione kuwa kuna haja ya kuongeza miundombinu wezeshi.



.jpeg)
.jpeg)







Social Plugin