
Na Bora Mustafa, Arusha .
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amezindua mfumo wa kidijitali wa “Ongea na Waziri” katika Hospitali ya Wilaya ya Arusha (Mount Meru), mfumo unaolenga kuwasogeza wananchi karibu zaidi na viongozi wa sekta ya afya.
Kupitia mfumo huo, wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Afya kwa kupiga simu bure au kutuma ujumbe wa maandishi kupitia namba 199.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Januari 26,2026 Waziri Mchengerwa amesema teknolojia ni chombo cha kuokoa muda na rasilimali za wananchi, na siyo lengo lenyewe.
Aidha, Waziri amepongeza maboresho ya huduma katika Hospitali ya Mount Meru ikiwemo kuanzishwa kwa online booking, kuimarika kwa huduma na ongezeko la imani kwa wananchi pamoja na uwepo wa huduma za VVIP zinazohudumia hata watalii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Amos Makalla, amesema ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Selian umewezesha wananchi kupata huduma za matibabu ya moyo ndani ya mkoa wao, mafanikio yaliyotokana na jitihada za Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Kwa upande wa Dkt. Lukumay amesema Hospitali hiyo pia imepata ithibati ya kimataifa ya daraja la nne, hatua inayoonesha ubora wa huduma zake.
Waziri ameeleza kuridhishwa na mpango wa ujenzi wa jengo ghorofa litakalopunguza msongamano wa wagonjwa, na kuagiza hospitali iongeze ubunifu ikizingatiwa kuwa Arusha ni jiji la kitalii.





Social Plugin