Na mwandishi wetu,Arusha
Mwenyekiti wa mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani kushirikiana na Serikali kuleta umoja wa kitaifa.
Katika kulitekeleza hilo, Mbowe amevitaka vyama vya upinzani kuweka utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa katika njia moja ya kuliunganisha Taifa.
Kauli hiyo ya Mbowe inakuja wakati ambao Rais Dkt Samia ameshafanya juhudi mbalimbali zinazolenga kuleta maridhiano ili kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa.
Mbowe ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu kwa niaba ya familia ya Mzee wakati wa maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei yanayofanyika mkoani Arusha.
“Tafuteni namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili katika utaratibu wa kuliunganisha Taifa, kusiwe na taifa la vipande vipande vya vyama vya siasa,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa
“Tunataka Taifa moja lenye misingi ya maendeleo, lenye upendo, lenye utengamano ili kuwezesha wale watakaokuwa na kwenye uongozi katika maeneo mbalimbali kufanya kazi zao kwa furaha na amani,” ameeleza Mbowe.

Social Plugin