Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AAGIZA HAYA KUMUENZI MTEI



Na Josephine Manasseh, Arusha

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya njia nne ya Tengeru hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kumuenzi Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei.

Katika hatua hiyo ya kumuenzi Mtei, mkuu huyo wa nchi ameagiza hadi Februari 20, mwaka huu maeneo yote korofi yarekebishwe kuwaondolea wananchi shida na kuleta maendeleo kama alivyotaka marehemu Mtei.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Rais Dkt Samia, jijini Arusha leo, Jumamosi Januari 24, 2026 wakati wa salamu za mwisho kwa Gavana wa kwanza wa Tanzania, Mtei.

Ameitaka Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kukamilisha kazi hiyo kwa haraka kama alama kwa Mtei aliyeitumikia nchi kwa uadilifu, heshima na kiu ya maendeleo.

Pia, ameagiza katika Shamba la Mringa Estate ambako mchakato ulielekeza baadhi ya wananchi wanufaike ni muhimu wahusika wote wanaostahili wapate haki zao, kwa kuwa Mtei alipenda haki.

Agizo lingine, ametaka maeneo ya kufanyia biashara ndogondogo yenye miundombinu mibovu mkoani Arusha, Mkuu wa Mkoa ayabaini na zipelekwe fedha kuyaboresha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com