

Na Kadama Malunde – Shinyanga
Shule ya BECO Pre and Primary School iliyopo Shinyanga Mjini imeendelea kung’ara kitaifa baada ya kufanya vyema katika matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2025, ambapo wanafunzi wote 20 waliofanya mtihani huo wamepata Daraja ‘A’ bora.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), shule hiyo yenye namba ya usajili PS1704060 imepata wastani wa 280.9 na kufanikiwa kuwa miongoni mwa shule bora zaidi nchini Tanzania.
Matokeo hayo yanadhihirisha ubora wa BECO katika kutoa elimu bora na yenye ushindani mkubwa. Wasichana 9 na wavulana 11 wote wamepata daraja ‘A’, jambo linaloifanya shule hiyo kuwa na ufaulu wa asilimia 100 kwa kiwango cha juu zaidi.
Mafanikio hayo yametokana na juhudi kubwa za walimu, ushirikiano wa wazazi na nidhamu ya wanafunzi.
“Tunajivunia sana matokeo haya. Kila mwaka tumekuwa tukipanda zaidi kitaifa na matokeo ya mwaka huu yamethibitisha ubora wa BECO kama shule ya mfano nchini,” umesema uongozi wa shule.Tangu mwaka 2021, BECO imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya kitaifa ambapo ilishika nafasi ya 10 kitaifa, na kuendelea kuwa miongoni mwa shule zenye matokeo bora mwaka 2022, 2023, 2024 na sasa 2025.
Shule hiyo inasifika kwa kuwa na mazingira bora ya kujifunzia, walimu wenye weledi, mafunzo ya maadili mema, huduma ya usafiri wa uhakika na ada nafuu inayomuwezesha kila mzazi kumpatia mtoto wake elimu bora.
BECO Pre and Primary School inapatikana Shinyanga Mjini, nyuma ya Kom Sekondari, na inaendelea kupokea wanafunzi kwa madarasa ya Chekechea, Darasa la Kwanza na wanaohamia madarasa mengine.
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 0763 157 400 | 📞 0624 293 323
BECO – The Home of Bright Children! 🌟
Social Plugin