Mdau wa maendeleo ambaye pia amewahi kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Eustard Athanace Ngatale (aliyevaa suti) amekabidhi msaada wa kompyuta moja katika Shule ya Sekondari Mwasele iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Ngatale amesema mchango huo ni sehemu ya jitihada zake za kusaidia kuimarisha elimu na kuongeza ufanisi wa wanafunzi na walimu katika matumizi ya TEHAMA shuleni.
Aidha, amewataka kuitumia kompyuta hiyo kwa masomo na utafiti badala ya mambo yasiyo na tija, huku akisisitiza kuwa elimu ya sasa haiwezi kutenganishwa na matumizi ya teknolojia.
Uongozi wa shule pamoja na wanafunzi wamemshukuru Mhe. Ngatale kwa msaada huo wa Kompyita na kuahidi kutunza na kutumia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Social Plugin