
Aliyekuwa mtia nia ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Eustard Athanace Ngatale, ameungana na wananchi, wanachama na makada wa CCM katika kampeni za uchaguzi jimbo hilo kumnadi mgombea ubunge wa CCM, Mhe. Patrobas Katambi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Old Shinyanga, Ngatale ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI, amewataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwa kupiga kura kwa wingi ifikapo Oktoba 29, 2025.
“Nawasihi wananchi mjitokeze kwa wingi kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Patrobas Katambi kuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini, pamoja na madiwani wa CCM ili tuendelee na safari ya maendeleo,” amesema Ngatale.
Aidha, amehamasisha mshikamano na ushirikiano wa wanachama na makada wa CCM katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo Shinyanga Mjini, akibainisha kuwa CCM ndiyo nguzo pekee ya maendeleo ya wananchi.



Social Plugin