Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AHMED SALUM ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA SPIKA MSTAAFU JOB NDUGAI

 

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Ally Salum, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Aliyekuwa Spika Mstaafu wa  bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Job Yustino Ndugai, kilichotokea tarehe 06 Agosti 2025.

Kwa hakika taifa limepoteza kiongozi shupavu, mwenye hekima, busara, na mchango mkubwa katika kuimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora. Mhe. Ndugai alikuwa kielelezo cha uzalendo, uvumilivu na uadilifu katika utumishi wa umma.

Mhe. Ahmed Ally Salum anatoa pole kwa familia ya marehemu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), wananchi wa Kongwa, pamoja na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa.

Aidha, anamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

“Tutamkumbuka daima kwa uongozi wake uliotukuka na moyo wake wa kizalendo.”

Imetolewa Na.

Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la solwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com