Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JOSHUA NASSARI AJITOSA TENA UBUNGE ARUMERU MASHARIKI

 


 Na Woinde Shizza, Arusha 

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari, ameibuka rasmi katika kinyang’anyiro cha kuwania ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, safari hii kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nassari, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alifika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arumeru akiwa na fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kikongwe ili kurejea tena bungeni kwa mara nyingine.

“Nimerudi nyumbani. Nia yangu ni moja tu kuwatumikia wananchi wa Arumeru Mashariki kwa ufanisi mkubwa zaidi, kwa kutumia uzoefu nilioupata ndani na nje ya siasa, pamoja na kujifunza kwa vitendo namna serikali inavyofanya kazi,” alisema Nassari akiwa nje ya ofisi za chama.

Kwa hatua hiyo, Nassari amejiunga rasmi na kundi la makada wa CCM wanaowania kupitishwa kugombea ubunge kupitia kura za maoni ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.


Nassari aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kupitia Chadema na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa kabla ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Wilaya. 


Kurudi kwake kwenye siasa za ubunge kupitia CCM kunachukuliwa kama hatua ya kipekee inayoweza kuleta mvuto mpya katika mchakato wa ndani ya chama hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com