
Kikundi cha Yanga Police Jamii Fitness kutoka Shinyanga kimeandaa "paredi ya supu" kama sehemu ya kusherehekea ushindi wao mkubwa wa Yanga SC kutwaa ubingwa mara ya nne mfululizo.
Wanachama wa kikundi hicho wamekusanyika kwa mazoezi ya pamoja kisha wakajumuika kwa supu ya nguvu, ikiwa ni ishara ya furaha na mshikamano baada ya mafanikio yao ya kihistoria.
Mmoja wa viongozi wa kikundi hicho amesema kuwa "paredi ya supu" ni utamaduni wao wa kipekee wa kusherehekea ushindi na pia kuhamasisha afya na umoja katika jamii.

Social Plugin