Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MARIDHIANO YATATUPA AMANI YA KUDUMU- WANANCHI



Na Mwandishi wetu

Watanzania wamehimiza utayari wa Jamii na makundi mbalimbali kushiriki katika mchakato wa maridhiano, wakisisitiza kuwa maridhiano ni silaha muhimu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali inayotokea katika jamii kwani maridhiano ndiyo kitovu cha upatanishi kwa Taifa.

Wito huo umetolewa kufuatia kauli zilizotolewa mara kadhaa na Rais Samia Suluhu Hassan, aliyesisitiza kuongoza mchakato wa maridhiano ya Kitaifa ili kuwa na mwelekeo wa pamoja kama Taifa na zaidi katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Baadhi ya wananchi hao akiwemo Bw. Ridhiwan Hamidu Muhimu na Mansour Bakari, wakazi wa Ilala Jijini Dar Es Salaam wamezungumza nasi na kusisitiza kuwa chuki na magomvi si utamaduni wa Watanzania na maridhiano yatamfanya kila mmoja kupata kile anachostahili.

"Maridhiano yatapelekea kila mmoja kupata kile anachokistahili. Bila ya mazungumzo hatutoweza kufikia kwenye hali nzuri, bila ya maridhiano hatutakuwa na amani ya kudumu nchini." Amesisitiza Bw. Ridhiwan.

Bw. Bakari pia amezungumzia kuhusu ghasia za Oktoba 29, 2025 akisema maandamano haramu hayawezi kusaidia katika utatuzi wa changamoto na badala yake huzaa athari nyingi zaidi ambazo zimekuwa zikiwaathiri wananchi wa kawaida badala ya kuleta jawabu kwenye changamoto.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com