MUSA RYOBA ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA UBUNGE TARIME MJINI
Tuesday, July 01, 2025
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Musa Ryoba, ameonesha dhamira ya kulitumikia Taifa kwa kuchukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, mkoani Mara, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025. Ryoba amechukua na kurejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Tarime.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin