
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Alex Frank maarufu kama Mr. Black, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.
Mr. Black ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi na Vijana Wilaya ya Shinyanga Mjini, mjumbe wa Baraza la Vijana, pamoja na kuwa mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya The BSL Investments Company Limited pamoja na taasisi za BSL Schools Tanzania na Rwanda
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Mr. Black amesema ana nia ya dhati ya kuiinua Kata ya Kizumbi na kuiweka kwenye ramani ya dunia kupitia ubunifu, maendeleo ya kijamii, kuinua uchumi wa wananchi na kusimamia utawala bora.
Aidha, ametoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa uongozi wake thabiti na juhudi endelevu za kuijenga Tanzania mpya yenye dira ya maendeleo kwa wananchi wote.
Social Plugin