Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria katika Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Eustad Ngatale, ameonyesha dhamira ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa kuchukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo.
Ngatale amekamilisha mchakato huo katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, akionesha uzito wa nia yake ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 kupitia tiketi ya CCM.
Social Plugin