Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Michael Kishiwa Francis Kapale, leo Juni 28, 2025, amefika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, na kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania Ubunge wa Jimbo la Kishapu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kapale amesema ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kwa moyo wa uzalendo na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kishapu kwa kujikita katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, sambamba na kuisimamia vyema Ilani ya CCM.
Social Plugin