
Mhandisi Johnston Johansen Mutasingwa amechukua fomu ya kuomba ridhaa CCM kugombea ubunge Jimbo la Bukoba mjini leo Juni 28,2025.
Eng. Johnston Johansen Mutasingwa, Huyu ni kijana machachari, na ni msomi, ana Shahada ya uhandisi Ujenzi (Civil Engineer).
Kwenye masuala ya siasa, Injinia Mutasingwa si mgeni! Ni mwanachama kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mathalan, ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya, kutoka kwenye kata yake ya Kibeta, mwaka 2015 na 2020 alichaguliwa kushiriki kampeini za Chama kwa njia ya mtandao. Pia mwaka 2020 baada ya uchaguzi aliteuliwa kuwa mlezi CCM kata ya Kahororo
Mwaka 2020 alitia nia kugombea ubunge. Kwenye kura za maoni alishika nafasi ya 12 kati ya wagombea 57. Matokeo hayo yaliyomtia moyo, pamoja na mambo mengine, yalitokana na uaminifu na utiifu wake kwa chama (CCM).
Kadhalika, Injinia Johnston Mutasingwa ana kipaji cha uongozi. Kwa sasa, kazini kwake ni kiongozi kwenye vyama vya wafanyakazi na taasisi ya ujenzi na migodi (TAMICO) na ni Mjumbea wa kamati kuu tendaji taifa(KUT) na mjumbe wa kamati ya fedha Taifa,Vilevile, anakaimu ukuu wa kitengo cha Mipango( Planning), TANROADS, Kagera. Pia, ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi TANROADS kitaifa, akiwa mwakilishi kutoka mkoa wa Kagera.
Injinia Mutasingwa ni kijana mpenda maendeleo, usawa kwa wote na amejaaliwa kutokuwa na makundi. Kwa vile jimbo la Bukoba Mjini lipo kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya miundo mbinu, kura zikitosha, upele utakuwa umepata mkunaji! Maana kwa miaka kadhaa, amesimamia kwa ufanisi miradi mingi ya TANROADS ya ujenzi na matengenezo ya kawaida, Madaraja( mf.Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140) makubwa na ya dharura, ya barabara katika mkoa wetu wa Kagera.

Social Plugin