Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. SHONYELA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE UYOLE


Daktari Seria Masole Shonyela akionesha ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Uyole, jijini Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutoka ofisi za CCM jimbo la Uyole jijini Mbeya.

Na Regina Ndumbaro-Mbeya

Dkt. Seria Masole Shonyela, ambaye ni Daktari wa Wanyama katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ameweka wazi nia yake ya kisiasa kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Uyole, jijini Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Seria amesema amejizatiti kuleta mabadiliko chanya Uyole kwa kutumia uzoefu wake katika sekta ya mifugo, afya ya jamii na maendeleo ya kijamii.

Ameahidi kushirikiana na wananchi kwa karibu endapo atapewa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge wa jimbo hilo.

Daktari Seria Masole anatajwa na wengi kama mtaalamu mwenye weledi na mchapa kazi na mzoefu wa kufanya kazi na wananchi ambaye amejipambanua kwa kuwahudumia wafugaji kwa karibu na kushiriki kikamilifu katika kampeni za uhamasishaji wa afya ya mifugo.

Uamuzi wake wa kuingia kwenye siasa unaonekana kama jitihada za kupanua wigo wa utumishi kwa jamii kupitia nafasi ya uongozi wa kisiasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com