Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GILITU MAKULA AINGIA RASMI KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE SHINYANGA MJINI, 'AMECHUKUA FOMU'

Mfanyabiashara maarufu na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gilitu Makula, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama chake – CCM.

Tukio hilo limefanyika leo tarehe 28 Juni 2025 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Chama Cha Mapinduzi kimefungua rasmi mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu za kugombea udiwani, ubunge, na uwakilishi kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025. Mchakato huu umeanza rasmi Juni 28, 2025, na unatarajiwa kufungwa Julai 2, 2025.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com