Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FAHAD MUKADAM KUVUNJA UKIMYA? MINONG’ONO ANAGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT-WAZALENDO


Kumekuwa na minong’ono ya chinichini katika duru za kisiasa kuwa Fahad Gulamhafiz Mukadam, mtoto wa mwanasiasa mkongwe Mzee Gulam Gulamhafiz Mukadam ambaye ni Kada Kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anapanga kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu utaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Ingawa bado hakuna tamko rasmi kutoka kwake wala chama husika, vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa maandalizi ya awali yameshaanza kwa hatua za kimkakati chini kwa chini. 

Hatua hii, iwapo itathibitishwa, huenda ikatikisa anga ya kisiasa na kuibua mjadala mpana ndani na nje ya chama hicho chenye ushawishi unaokua miongoni mwa vijana.

Endelea kufuatilia – tutazidi kukuletea habari zaidi...

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com