Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NTOBI AUTAKA UBUNGE SHINYANGA MJINI KUPITIA ACT-WAZALENDO... TAYARI KACHUKUA FOMU

Naibu Waziri Kivuli,Habari,Mawasiliano na TEHAMA Emmanuel Ntobi,(kulia)akikabidhiwa Fomu ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na Katibu wa ACT-Wazalendo Jimbo hilo Justa Denis.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Naibu Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Emmanuel Ntobi, leo Juni 30, 2025, amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama hicho.

Ntobi amekabidhiwa fomu hiyo katika Ofisi za ACT-Wazalendo za Jimbo la Shinyanga Mjini na Katibu wa Jimbo, Justa Denis.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, Ntobi amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini, atahakikisha anawatumikia wananchi kwa uaminifu, kuleta maendeleo na kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com