
Jina langu ni Hamadi Murimi, mwanaume ambaye maisha yake ni shuhuda wa ukweli kwamba kila chaguo tunalofanya katika maisha huturudia na wakati mwingine kuamua hatima yetu bila ya sisi hata kupenda.
Kwa muongo mmoja, nilibarikiwa kuwa na mwanamke mmoja mzuri ajabu sana ambaye kusema kweli alikuwa ni mwanga wa upendo na utulivu katika maisha yangu.
Hata hivyo, kutokana na udhaifu kama mwanaume kuna wakati nilipotoka na kutoka kwenye njia. Nilimsaliti, na kwa kufanya hivyo, nilivunja utakatifu wa ndoa yetu. Kubainika kwa uovu wangu huo ambao ulipelekea kupata watoto wawili nje ya ndoa, kuliashiria mwanzo wa anguko.
Social Plugin