Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KITUO CHA MAFUTA"TINTOBER PETROL STATION"CHAZINDULIWA RASMI SHINYANGA


Meneja wa Kituo cha Mafuta cha Tintober Petrol Station, Peris Jackton akimuwekea mafuta bodaboda wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KITUO kipya cha mafuta cha Tintober Petrol Station, kimezinduliwa rasmi leo Mei 10, 2025, kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani.
Kituo hicho kipo barabara ya kuelekea Old Shinyanga, mbele kidogo baada ya Shule ya Sekondari KOM, ambapo wateja wameanza kupata huduma ya mafuta mara baada ya uzinduzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi,Meneja wa kituo hicho, Bi. Peris Jackton amewashukuru madereva na wakazi wa Shinyanga kwa kujitokeza kwa wingi, huku akiwaomba waendelee kufika kituoni hapo kwa ajili ya kuendelea kupata huduma bora na za uhakika.
“Nawaomba wananchi wa Shinyanga waje kwa wingi kwenye kituo chetu cha mafuta na kupata huduma bora," amesema Peris.

Nao baadhi ya Madereva, wameshukuru Kituo hicho cha Mafuta kuzinduliwa, kwamba wamesogezewa huduma karibu.
Kauli mbiu ya Tintober Petrol Station ni: "Ubora wa mafuta kwa kila tone."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com