

Ujumbe huo uliandikwa na hayati Papa Francisko siku chache kabla ya kuaga dunia na ulikabidhiwa kwa Rais Samia na Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino.
Kupitia ujumbe wake kwa umma, Rais Samia amesema:
"Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote, aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino. Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema."
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuendelea kumkumbuka hayati Papa Francisko katika sala na kumuombea apumzike mahali pema.
Hayati Papa Francisko atakumbukwa na Watanzania kwa mchango wake mkubwa katika kuhimiza imani, amani, mshikamano, na upendo miongoni mwa watu wote duniani, hususan bara la Afrika.
Imeandaliwa na Malunde 1 blog


Social Plugin