
Hayo yamebainishwa Februari 22, 2025 na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira vijijini RUWASA mkoani Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela wakati wa hafla ya uzinduzi wa kupokea mabomba yatakayotumika kusambaza maji iliyofanyika kwenye kata ya Nyamilangano jimbo la Ushetu.
Akisoma taarifa ya mradi huo Mhandisi Payovela amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa matangi 3, vituo 35 vya kuchotea maji, ujenzi wa ofisi ya mradi, uchimbaji na ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 43.8, ununuzi wa magari 2 na pikipiki 2 kwaajili ya usimamizi wa mradi.
"Mpaka sasa jumla ya kilomita 105 za bomba zimekwisha nunuliwa na mkandarasi na kilometa 66 za bomba za plastiki zimeshasambazwa kwenye eneo la mradi, faida za mradi huu utakwenda kuhudumia wananchi 100,089 kutoka kata 11 za Ushetu, utasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara, kipindupindu na homa ya matumbo wa wananchi kutokana na uwepo wa huduma ya maji safi na salama, aidha utasaidia kupunguza mimba za utotoni na utoro mashuleni kutokana na kutafuta maji umbali mrefu mradi huu unaotarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 06, 2026", amesema Mhandisi Payovela.
Akieleza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji ndani ya halmashauri ya Ushetu Mbunge wa jimbo hilo Dkt. Emmanuel Cherehani kukamilika kwa mradi huo kutapunguza adha ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na kuiomba serikali kuendelea kulitazama jimbo hilo.
"Mradi huu ulikuwa ni kilio cha wana Ushetu kwa takribani miaka 20, kutoka kilometa 40 manispaa ya Kahama tunapokea mabomba yatakayo sambaza maji kwenye vijiji vyetu 54, tunaishukuru serikali yetu kwa kutoa fedha hizi, ukikamilika mradi huu tutakuwa tumebakiza kata 9 na vijiji 58 ambavyo bado vitakuwa havijafikiwa na huduma ya maji, tumuombe Rais wetu aendelee kututazama wananchi wa Ushetu ili changamoto ya maji iwe historia kwenye jimbo hili", amesema Cherehani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amesema serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwenye sekta ya maji , barabara, umeme n.k.
Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndg. Mabala Mlolwa amesema ni furaha kubwa kuona ilani ya chama hicho inaendelea kutekelezwa kupitia Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba kero ya maji ndani ya jimbo la Ushetu ilikuwa ni ya muda mrefu lakini sasa inakwenda kuwa historia kwa wananchi.
Pia ameipongeza Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA mkoani Shinyanga kwa kusimamia miradi ya maji kikamilifu ndani ya mkoa huo.







Social Plugin