
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Venant Protas amekutana na viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Tura pamoja na mabalozi wote wa kata hiyo.
Katika mkutano huo, amechangia mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Tura, akionyesha kujitolea kwa maendeleo ya chama na jamii.
Aidha, Mheshimiwa Mbunge amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Tura, ambapo alikusanya maoni na kero za wananchi.
Katika mkutano huo, amejitolea mchango mkubwa kwa jamii, akichangia mifuko 50 ya sementi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki moja, bati 60 zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili, na shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Tura.
Pamoja na hayo, ametoa shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa banda la bodaboda la kupumzikia, akionesha kujali ustawi wa wafanyabiashara wadogo.
Ziara ya Mheshimiwa Venant Protas inaendelea kwa kukutana na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Jimbo la Igalula, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha maendeleo na ushirikiano wa kisiasa katika jimbo lake.

Social Plugin